Alhamisi, 26 Oktoba 2017

JARIDA MAARUFU NIRIA LAMPA SHAVU PETER

Jarida la Vibe.ng kutoka nchini Nigeria limempa shavu msanii wa muziki Peter aliyekuwa moja ya memba wa kundi la P-Square, linalounda na yeye pamoja na pacha wake Paul. Kupitia jarida hilo linalotarajiwa kutoka hivi karibuni, Peter ama Mr.P amefunguka mengi ikiwemo kutochanganya biashara na masuala ya familia, vile vile ameelezea juu ya kuvunjika kwa kundi hilo ambalo limefanya kazi kwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10. “One thing I will never do when I come back to this life again is mix family with business,” Peter Okoye, now known as Mr P, says as he discusses the break up of P-Square,’’ ameleza Peter kupitia jarida hilo la Vibe. Kwa sasa Peter anafanya kazi zake binafsi na amesha achia video yake ya kwanza iitwayo ‘Cool It Down’wiki moja iliyopita. Baadhi ya picha zinazopatikana katika jarida hilo.

Alhamisi, 21 Septemba 2017

NICKY MINAJ KAINGIZA RASMI BIDHAA YAKE YA LIPSTIC SOKONI

Rapper wa kike kutoka Young Money Nicki Minaj amekuja lipstik yake baada ya kutangaza kuachia rasmi bidhaa zake hizo sokoni mwezi huu. Nicki ambaye alitangaza kuachia bidhaa hizo mwezi uliopita kupitia kampuni ya M.A.C amefanya hivyo kwa kuachia aina mbili za lipstick ambazo ni NickisNude na ThePinkprint, zitakazouzwa kuanzia dola 18 sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi elfu arobaini ivi za kibongo 40,000\= “Ok I’m about to announce my winners on twitter. This might be the illest gift set I’ve ever seen. My fans deserve it. They’re gonna be so happy. But mad jealous too if they don’t win. Awww @maccosmetics you’re getting like 20 lipsticks and 2 glosses. Yikes. Plus my signature colors #ThePinkprint & #NickisNude We’ve officially launched in the US!!!!!!,” ameandika mrembo huyu kupitia mtandao wa Instagram.
uwekezaji uleta matokeo mazuri ra badae ata TANZANIA tumemuona Nasibu Abdul Diamond akiwa msanii wakwanza Tanzania kufanya uwekezaji mkubwa katika perfume zake aina ya Chibu perfume na Karanga , ambapo bidhaa zote zinaonyesha kufanya vizuri sokoni , msanii mwingne kutoka bongo ambaye ame anauwekezaji kama huo ni Joh makini ambae bado haijawa officil ila ana tarajia kuachia condom zake MAKINI condom

HIP HOP YANGU INAPEDWA KULIKO WANAOJIITA WANA HIP HOP; NAY

Msanii wa muziki wa Bongo, Nay wa Mitego wamejitapa na kujivunia style yake ya muziki anayofanya licha ya baadhi ya wasanii wenzake kumuondoa katika kundi la wasanii wa hip hop. Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuondolewa katika kundi la muziki wa HIP HOP hakumuumizi kwani anaangalia biashara na wasanii wanatakiwa washindane katika eneo hilo. “Muziki wa HIP HOP unahitaji vitu ambavyo vinaishi, tuzungumzie maisha ya watu ya kila siku. Utaona wanasema Nay siyo mwanahip hop, wananitoaga kwenye kundi la hip hop lakini why ndio na mashabiki wengi kuliko wao, why nimekuwa napendwa kuliko wao, why angalau na vijihatua kuliko wao?” amesema Nay. “Ni kwa sababu nafanya kitu cha Watanzania nafanya kitu ambacho kipo kwa wakati huo na ndivyo tunatakiwa kufanya ili isionekane kila siku waimbaji ndio wana mkwanja, tushindane. Marekani wasanii wenye hela nyingi ni wanahip hop kwanini na sisi tusiweze hivyo,” ameongeza. Kwa mwaka huu Nay wa Mitego ametoa ngoma kama Wapo na Moto ambazo zipo katika style ya rap, huku ngoma kama Makuzi na Acheze zikiwa katika style ya kuimba. NAY ni moja ya wasanii ambao walianza na muziki wa HIP HOP kutokana na ugumu kwamba mziki huo hauna soko hapa bongo na kuanza kuimba imekua changamoto kubwa kwa wasanii wengi sana nchini hapa asilimia 90 ya wasanii wa HIP HOP wamebadilisha muziki wao kwa madai muziki huo haulipi , miongoni mwa wasanii walio wahi kuchana ila sasa ni waimbaji ni MADEE, DIAMOND, DULLY SYKES, RAYVANNY, NA wengine wengi ila wachache kama FID Q, CHINDO, wanaonekana kua baadhi wasanii walio baki kwenye misingi ya HIP HOP BONGO

MADEE NA DOGO JANJA KUJA NA ALBUM YA PAMOJA ; MADO

Wasanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee na Dogo Janja wana mpango wa kutoa albamu ya pamoja.kabla ya mwaka huu kuisha . Dogo Janja ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa album hiyo itakwenda kwa jina la Mado ikiwa ni muunganiko wa majina yao na wanatarajia kuitoa November mwaka huu. “Album itakuja inaitwa MADO
ni yangu na na Madee, unajua album ni stori, ni kama kitabu unatakiwa ukisikiliza uelewe, siyo tu nyimbo ndio maana ukifuatilia Machozi, Jasho na Damu imeelezea tu,” amesema Dogo Janja. Mwaka huu tumeona baadhi ya wasanii wa bpngo flava wakijinadi kutoa album swala ninalo lisubiliwa kwa hamu na watu wengi, mimi kama mdau wa muziki nafurahi kuckia ivyo ,miaka ya hivi karibuni album zimeonakana kua ngumu sana kuuzika yote kutokana na teknolojia ya internent kurahisisha mfumo wa upatikanaji, miongoni mwa wasanii walio dhibitisha kutoa album mwaka huu ni pamoja na CHEGE CHIGUNDA, FID Q , ROMA NA STAMINA,NA BARNABA mashabiki tunasubili kwa hamu kubwa ujio wa hizi album .

Jumatano, 20 Septemba 2017

WASANII BONGO NA UPENDO WA MACHONI

Prodyuza wa THT, Emma The Boy, ambaye alipotea kwa takribani siku tano ila kwa sasa ameshapatikana, lakini cha ajabu wasanii wa Bongo fleva walikaa kimya, kama vile hawajui au haiwahusu, jambo hili linaonyesha wazi ndani ya tasnia yenu kuna ubaguzi. Maswali ninayojiuliza hadi sasa ni kwanini alivyotekwa Roma mlihangaika usiku na mchana? Mkapaza sauti zenu kupitia mitandao yenu ya kijamii na mkashinda vituo vya polisi na mahospitalini? Mkaitisha mkutano wa kujadiliana juu ya nini cha kufanya?, kwa takribani siku mbili hakukuwa na stori nyingine zaidi ya huzuni tu. Na kwa kiasi kikubwa zenu zilizaa matunda na hatimaye Roma, moni na bin laden wakapatikana, ndiyo maana kwa kulitambua hilo kupitia ngoma yake za Zimbabwe akawashukuru wale wote waliopaza sauti zao. Lakini juhudi hizo mlishindwa kuzionyesha kwenye tukio la Emma The Boy, ambalo linafanana na lile la Roma, siyo mitandaoni, wala kikao cha kujadili mtampata wapi, ndiyo kwanza mpo bize na mambo yenu, kwani yeye na Roma wana tofauti gani?, ni kwamba taarifa hamkuzisikia au haikuwagusa ndiyo maana mliwasusia wasanii wa THT tu, wakiwemo Ditto, Amini na Barnaba ndiyo wahangaike peke yao?, nlichogundua ni kama umoja wa usoni tu ila moyoni hamna kitu nakumbuka pia kifo cha NGWEA kila mtu aliuzunika na mlijitolea kweli ajabu ni kifo cha LANGA ambacho kilikua siku kadhaa tu baada ya kifo cha Ngwea lakin cha ajabu mapokeo hayakua kama ya Albert Mangwea , tasnia yetu ina shida flani ambayo hatuijui sema mungu atusaidie lipite mbali Neno langu co sheria, lakin poleni kama nimewakela

LISU INABIDI APELEKWE MAREKANI; NYALANDU

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweka kambi nchini Kenya kuangalia uwezokano wa kupata ruhusa kutoka kwa madaktari ya kumsafirisha Mh Tundu Lissu kwenda Marekani kwaajili ya matibabu zaidi baada kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Nyalandu amedai ni siku ya tatu bado hajapata ripoti inayoonyesha maendeleo ya mgonjwa huyo ili waangalie kama wanaweza kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi. Taarifa ya Mh Nyalandu Tumekuwa Nairobi Hospital tukisubiri madaktali watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissukupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospitalwangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo

Jumatatu, 17 Julai 2017

MCHORO WENYE DHAMANI KUBWA KUWAHI KUTOKEA DUNIANI

Kama wewe ni mbukuzi kama mimi hapa nadhani ushawahi kusikia au kuona (kwenye runinga) mchoro maarufu wa MONALISA mchoro wenye dhamani kubwa sana Dunia nzima ambao watu husafiri kutoka nchi mbali mbali kwenda kuuona nchini ITALY katika makumbusho ya LOUVRE ambapo unadhamani ya Dolla millioni 785 iv , ni pesa nyingi sana , na watu mbali mbali husafili kwenda Ufaransa kuuona , una ulinzi wa Hali ya juu kwani watu kadhaa walijalibu kuuiba miaka ya nyuma . Mchoro huu ndo mchoro maarufu sana kuwahi kutokea Duniani ..

HISTORIA FUPI
Mchoro wa MONALISA ulichorwa na Leonardo Da Vinci raia wa Italy aliezaliwa 15.4.1452 hukoo nchini Italy , Leonardo ni moja ya watu makini kuwahi kutokea duniani kwani ana nadhalia zake ambazo mpaka kesho zinatumiwa sana duniani , hakuwa tu mchoraji pia alikua Mwanasayansi, Mwanahisabati, Mwanamuziki, na fani nyingine mbali mbali ndo maana wahenga kama mimi tunamuona ni moja ya ma geneus kuwahi kutokea , ikumbukwe Leonardo ndo mtunzi au msimamizi wa Nadhalia ya sayansi ya kitu kupaa angani bila kushika mahali na ndo maana hufananishwa sana na watu kama Isaac Newton, Albert Einstein, Galileo Socrates n.k Uchoraji wa picha ya MONALISA ulianza mwaka 1503 mpaka 1506 , alipoukamilisha kwa kiasi kikubwa sana , mnamo mwaka huo huo alihamia Ufaransa na kuendelea na makazi yake kule , mchoro wa MONALISA haukua mchoro wa siku wiki au mwez ulichukua mda sana , kwakua Mchoraji Leonardo alikua akijihusisha na mambo mengi ilimchukua mda sana na inaaminika ndo sababu ya picha kua nzuri adi kesho kutwa kwani ilichukua mda sanaa. Mnamo tarehe 2.5.1519 umauti ulimfika Leonardo Da Vinci mchoraji wa mchoro wa MONALISA ulikua wakawaida sana ila vitu vilivyofanya mchoro huu kua special ni kutokana na mtu mwenyewe aliemchora kua special sana katika maisha ya kawaida ..

Baada ya miaka 300 baada ya kifo cha Leonardo picha ilianzakujipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na ustadi uliokua umetumika kuichora picha ile ule upekee wa picha na uhalisia uliifanya picha ile kuonekana special sana karne ya 19 watoto wa wafalme mbali mbali duniani waliitumia picha ile km mifano ya wanawake ambao wanatamani kuwaowa .

Salai mwanafunzi wa Leonardo alitumia picha ile kujipatia kipato kwa kuionyesha sehemu mbali mbali mnamo karne ya 19 watu mbali mbali walisafiri kwenda kuiona picha iyo ilizidi kujipatia umaarufu mwaka 1963  Rais wa Marekani kwa kipindi kile John F. Kennedy aliiomba picha iyo iende marekani na ililindwa sn na kukatiwa bima ya dolla million 600 , iliwasili nchini Marekani Washingtoni DC na watu na misululu miref ilisimamwa pale watu kuishika tu na kila mtu aliishika kwa sekunde 15 tu . Mwaka 1964 nchi kama Japani na USSR ,nazo zilizidi kuipa umaarufu sana picha ile kwani ilitakiwa kuenda pia kwa nchi hizo.

UPEKEE WA PICHA

1;Ndo ilikua picha ya kwanza ya rangi kuchorwa kwakipindi kile miaka ilipo chorwa.

2; Ulikua ni mchoro mzuri wa mtu wakusadikika ambae kila mwanaume alitamani kua na Mwanamke kama yeye na wakati hakuwepo wala hakuwahi kutokea

3; Picha ya MONALISA ilimuonyesha mwanamke mzuri ila hakuwa na Nyusi wala kidani chochote ila alikua mzuri sana .

4;Mchoraji mwenyewe Leonardo Da Vinci alikua ni moja ya ma genious wachache kuwahi kutokea Duniani .

5; Ndo picha yenye dhamani kubwa Dunia nzima adi hii leo

Iliwahi kuibiwa mwaka 1856 ila waliipata 1857 na watu wengi waliona kua picha iyo inadhamani kubwa adi hii leo inaulinzi wa bullet proof ndani ya makumbusho ya Louvre Paris nchini Ufaransa  .

By FOBES

ZIFAHAMU SEHEMU 5 JIJINI MWANZA ZENYE FURSA

Maendeleo jijini mwanza yanakua kwa kasi sana katika nyanja nyingi hasa kiuchumi na kijamii , maendeleo yanakua kwa kasi sana kila kukicha kwani Mwanza ya kitambo co sawa na Mwanza ya sasa mbali na Ziwa Victoria kua n moja ya vivutio vizuri kuwahi kuwepo jijini humo pia miundombinu imezidi kuboreshwa kila siku iendayo kwa Mungu . Ukirudi miaka mitano nyuma utakubaliana na mm kua Mwanza ya sasa imebadilika sana kwa nyanja mbali mbali barabara karbia zote mjini kati zina lami  hali inayozidi kuunyanyua uchumi kwa kasi sana..

Upanuzi wa barabara mbalimbali kati kati ya jiji umezidi kupendezesha na kurahisisha usafili hali inayopelekea kukua kwa uchumi jijini hapa , upanuzi wa barabara nne makongoro mpaka Airport unazidi kunogesha maadhali ya jiji letu au upanuzi wa barabara tatu  kati ya Mlango mmoja mpaka Igoma unazidi kufanya jiji kuonekana zuri kila kukicha. Leo ndugu yenu wa damu kabsa nmeamua kuwaleetea maeneo matano (5) ambayo ni vyepesi sn kuishi hasa mtu wa kipato cha kawaida au kipato cha chini . Ifuatayo ni list ya maeneo matano mepesi kuishi jijini Mwanza, na ntaanza na no 5 mpaka 1..


5: BUHONGWA
Hii ni seemu ya wilaya Nyamagana , pia ni kituo kikuu cha daladala zitokazo mjini kwenda Buhongwa , seem hii imechangamka sana pia inafursa za kazi na kujiajili.pia , kuna soko kubwa la mazao ya chakula na wakazi wengi wa eneo hili ni watu wa kipato cha chini kuanzia (500) unapata chakula na unaishi vizur ivyo kija yoyote , unaweza kuchukua km fursa iv ili kuendeleza harakati zako town...

4:IGOMA
Uku ni Wilaya ya Nyamagana kama kilometa 11 kutoka mjini kati , kuna machinjio kubwa Mwanza nzima ipo maeneo haya pia wepesi wa upatikanaji vitu ni mkubwa sn kwani kuna adi nguo za buku buku sharti nzuri tu unapata pia kuna uwepesi wa vyakula na fursa za ajira zipo nyingi sn kwani kuna viwanda vingi sn maeneo jiran km kijereshi na mnadani , mbali na fursa zilizopo pia ndo eneo ambalo linaongoza kua na wasukuma wengi sn jijini Mwanza , pia kuna mnada wa Ng"ombe na Mbuzi hali inayofanya pazidi kua na fursa nying za ajira , Vyumba adi elfu kumi unapata so km umechoka kukaa kwa Mama ni moja ya maeneo mazur sana kwa kuanzia maisha kwani kuna wepesi wakuishi ... 

3:PASIANSI NA MABATINI
Pasiansi ipo wilaya ya Ilemela ni eneo la makutano ya Kiloleli , Airport na Mjini kati kuna mihangaiko mingi sn usiku na mchana pia ni sehemu nyepesi kuishi kwani kuna miundombinu inayowakutanisha watu pamoja pia kuna Hotel kubwa km Lenana ambayo ni nyota tano , Mabatini ni km Kilometa 2 iv kutoka mjini ni sehemu nzuri kuishi kwa kipato chakuanzia maisha pia ni sehemu nzuri kuwekeza kama una mtonyo ivi,,  maisha yanawepesi sn kwani ata elfu kumi unapata chumba , so mdau ukimchoka mama.njoo uku kwetu, Ndo maana sisi tunapaita Califonia kwani pako km blooklyne iv au Los Angels

2:KIRUMBA
Eneo lipo maeneo ya Ilemela karbu kabsa na Ziwa victoria Km 2 kutoka mjini kati mbali ya kua ndo eneo ilipo soko kubwa la samaki jijini Mwanza ila pia ndo eneo lenye Garage nyingi na Hotel nying sn Kirumba huchangamka  24/7 , yaani masaa 24 ndani ya siku 7 za wiki kwa Mwanza hili ndo eneo ambalo la kwanza kwanza kua na Hotel na Disco la kisasa kabsa maeneo kama Villa Park Resort  La kailo ni moja ya sehemu nzuri kabsa za starehe kuanzishwa jijini hapa km umefika mwanza na una weweseka pakuwekeza njoo uku panakufaaaa sn....

Namba 1 ni NYAKATO NA NYEGEZI  Nyakato ni sehemu iliyochangamka sn jijini Mwanza mishemishe za hela ni kubwa na nyingi sana kwani wingi wa watu hufanya paonekane kama mbele yaani kuna stand kubwa ya magar ya mkoani pia kuna miundombinu mizuri kwani kuna barabara ya makutano kati ya Musoma , Mjini kati na Kilimahewa , ni moja ya sehemu nzur Mwanza, Nyegezi ni moja ya sehemu zilizochagamka kuanzia watu wenyewe na fursa zilizopo kuna stand ya magari ya mkoani hali inayoiyfanya kua na fursa nyingi sn za kujiajili na kuishi hasa km ni kijana unaeanza maisha, Kama mgeni lazma uenjoy sn au hata mwenyeji .

Kama ni mgeni jijini au mwenyeji najua ukifika maeneo hayo lazma ukubakiane na mimi , yapo maeneo mengi sana ila haya ni baadhi tu ya maeneo ambayo mimi nayakubali cku zote

Ijumaa, 3 Februari 2017

NYERERE NA UJAMAA UBEPARI NA MAGUFURI



Mambo mengi yametokea toka nchi ya Tanzania ipate Uhuru, Mwalimu J. K. Nyerere alikua mkombozi mzur sana katika Taifa letu na tunamshukulu sana kiukweli mazuri ni mengi sana aliyotufanyia, nchi yetu toka kwa Uingereza disemba 9,1961, ilikua n mapinduzi ya Amani kabsa na yalikua ni makubaliano baina ya Mwalimu J, k Nyerere na Malkia wa Uingereza kua ikifka Tarehe 3 12 1961, atakabidhi nchini ya Tanzania kwa Wa Tanzania  Mwalimu alijitahidi sana kutuandaa,, kwa kuzunguka nchi nzima, kuakikisha, tunajiandaa VYEMA kupokea Uhuru wetu na kujiendesha wenyewe ikumbukwe Adi Tanzania inapata Uhuru ilikua na wasomi 15 tu, km watu waliosomea vitu mbali mbali na pekee ambao walikua wanaweza kuandika na kuongea kiingereza vizuri...



Ilikuepuka mambo ya ujamaa ilimpidi Mwalimu kuanzisha vijiji vya ujamaa nakujitegemea kuepuka watu kijitenga na kujibagua pia ilimbidi atumie kiswahili km lugha ya Taifa letu kwani Tanzania kuna makabila zaid ya 120,  ambapo kila kabila lina lugha yake na ustaalabu wake, pengine asingetumia lugha moja na sisi leo tu ngekua kama Nchi nyingne zinazopambana kisa ukabila au, aliweka sera pia ya kumruhusu kila raia kua na changuo la dini pia, kila mwanafunzi alitakiwa asome mkoa wa mbali ili ajifunze mambo ya jamii nyingne nchini kwake..


Ujamaa ulikua mzuri sana na kila kijiji kijiji kilijitegemea kwan kila kijiji kilizalisha vyakula vyakutosha na kila mtu alitumia bidhaa za Tanzania tu, mnamo mwaka 1978 Nyerere alitangaza hali ya Hatari ya Vita na Iddi Amin Dada wa Uganda hali iliyoharibu hali ya hewa ya Watanzania kwani vijiji vyote vilisitisha kuzalisha na vijana kama nguvu Kazi, ndio walikua wanategemewa kwenye mapambano na ndio nguvu Kazi pia, kiukweli Vita (1978__1979) ilisimamisha na kuendesha sana uchumi nchini Tanzania, ilipofika mwaka 1983 hali ilizidi kua mbaya kwa raia hali iliyopelekea Mwalimu kuanza kuomba msaada nje ya Nchi, kumbuka Tanzania ilikua inatumia mfumo wa ujamaa kuendesha nchi na nchi nying zinasera ya ubepari, Ivyo ili usaidiwe na bepali lazima uwe bepali

Kufika mwaka 1984 Mwalimu hali ya nchi haikua nzur kabsa njaa ilikua ni kubwa sana, akaamua kuachia madaraka na kumkabidhi Ally Hassani Mwinyi japo haikua kwa kupenda pengne is ingekua ivyo na yeye asiachia madaraka km marais wengne wa AFRIKA kwani ubepari ni wa awamu kwa awamu, inapofika mwaka 1992 nchi inaruhusu vyama vingi,,,, Swali ni Je is ingekua Vita ya kagera Mwalimu asingeachia madaraka  mpaka leo tunapokezana na siasa ya uongo na kwel, #munguibarikiTanzania #MunguibarikiAfrica

Jumatano, 25 Januari 2017

GOOGLE NA TEKNOLOJIA YAKE MPYA YA MAGARI




Kampuni ya Google maarufu sana dunia, kwa mambo ya mtandao imejiingiza katika uwekezaji wa magari, magari hayo yapo kiteknolojia zaid kwan n gari linaloweza kuendeshwa bila ya dereva na lina uwezo waku sense vitu mbali mbali, kama magari ya polisi, ajali mbele na ata hatari inayoweza kutokea, Gari hili linatumia kompyuta kuendeshwa ata ukiwa ndani ya gari hilo hutumii usukani utatumia compyuta, uwekezaji huu umeleta CHANGAMOTO kubwa kwa makampuni kongwe nchini Marekani,..


Moja ya Kampuni ambalo limeonekana kuguswa na jambo hilo n Kampuni maarufu ya Ford, ambayo nayo imeahidi kuingiza sokoni gari zake aina iyo kwa mmujibu wa jarida la Fobes nchini Marekani, Ukuaji wa teknolojia umekua ukikua siku adi siku, ambapo umeelekea nchi zilizoendelea kua na changamoto sana katika biasharA za

Jumamosi, 21 Januari 2017

BILLIONEA KATIKA MAKAZI MAPYA



Tarehe 20/01 /2017 siku yakiistoria kwa Wamarekani kwani ndio Tarehe ambayo wamempata rais wao wa 45 Bilionea Donard Trump ambaye amaepishwa rasmi kama rais wa nchi iyo, ni furaha kwa Wamarekani japo asilimia kubwa ya wakazi wa nchi iyo awapend uwepo wake kwa kudai n mbaguzi na ana tabia mbaya za udhalilishaji, aidha kuna maandamano mkubwa yalifanyika punde alipo apishwa na asilimia kubwa ya watu ni Wamarekani weusi ambao hawapendi uwepo wake kama rais pia jana akukua na watu wengi kama ilivyokua kwa ma rais wa nyuma kwanza puli kua pametulia sana akukua na shamlashamla km miaka kadhaa Y obama na marais wengne

Wengi wanasema si rais mzuri kwani amekua akiwasema vbaya wanawake na hata watu weusi ambao kama walimsusia ivi, kwan asilimia kubwa ya watu waliokuepo walikua n wazungu wenyewe na wageni wengne, ametangaza kuanza Kazi lasmi Tarehe 23 /01/ jumatatu izi siku za mwisho wa wiki watu watumie kusherekea ushindi wake, pia rais aliepita ametuma maombi kwa wananchi wa Chicago kuwaulkza km wangependa awafanyie chochote, kwa kua sasa n raia wa kawaid kama raia wengne..

Kundi kubwa la wanawake zaidi ya lakimbili wanatalajiwa kufanya maandamano ya Aman jumamosi ya Tarehe 21 /01/ kumkosoa na kauli zake na kukumbusha ikiulu n mahali patakatifu na sio pango la walanguzi,

Alhamisi, 19 Januari 2017

HABARI KWA PICHA









CHA NYUMBANI ICHOOOO, WAMCHANGANI NA WAKIMATAIFA


Wamchangani haoooo kwenye ubora wao wako vizuri saiv ila ubora unhethibitika Zenji wamelegeza kamba uko sasa wanarudi kwao ya nyumban, 2016/2017   VODACOM PREMIER LEAGUE tunasubiri sisi watazamaji Mungu ibariki #Tanzania Mungu ibariki #Africa

KUMBE DODOMA NZURI KULIKO




Dodoma iyooo makao makuu ya serikali kiukwel panafaa kua makao makuu ya serikali pazuri ki muonekano na ata hali ya hewa ukiwa Dodoma, unaona tofaut ya asubuh, mchana na usiku yaan ucku unajua kwel usiku umefika kuna hali ya hewa flan iv kama umetoka Dar lazma uwahi kuoa kutokana Na kiubalidi fulani iv, mwaka jana Septemba Dr John Pombe Magufuli aliiambia serikali inabidi ihame na kwenda Dodoma kwan ndio makao makuu ya serikali kutokana Na kua ndo Center ya Tanzania kiukwel ukiwa Dodoma ni rahis sana kufika sehem yoyote Tanzania ata mpangilio wa miundo mbinu co sawa na jiji lolote adi kufika mwaka huu mwezi wa pili inabidi serikali iwe kule kwan ata kampuni lililopewa jukumu la kuboresha miundo mbinu CRCC chini ya mwenyekiti wake bwana Fengchao Meng adi mwezi wa Pili mwaka 2017 wanajukumu la kusogelea malengo ya serikali kwa hatua kubwa ili iweze kuhamia uko mapema, Wanao tarajiwa kuhama ni Mawaziri na Manaibu wote na ofisi zote za Tamisemi zimeagizwa kupeleka makao makuu huko mapema mwaka huu, pia kuna ujenzi wa uwanja mkubwa wa kisasa wa michezo, ikumbukwe wazir mkuu Kassim Majaliwa kasema tayar kashaamia Dodoma Mungu ibariki #Tanzania Mungu ibariki #Africa 

Jumatatu, 16 Januari 2017

UTANI WA JADI



Kazi unogeshwa na dawa mpira unogeshwa na utani na masihara kidogo japo kwa wengne hupenda kusema watu ila awapend kusemwa ndo mpira ulivyo, kla mtu utamani ashinde kila siku, kwa nchini kwetu uhacmu upo Simba na Yanga, uwa nafurah mechi zikiisha vijembe vya mashabiki na wadau hakika kila kitu kinawenyew  ndo maaana ckuiz tuna Bet

ARSENAL KUA CHINI YA DANGOTE





Tajili namba moja AFRIKA Aliko Dangote kutoka Nigeria mmiliki wa Dangote Group yenye kusifika hasa hasa kutoa Saruji yenye mabao makuu uko Nigeria ndio inayompa utajili na kumfanya bilionea ivi karbuni amefanya uwekezaji wa hali ya juu sana Nchin Tanzania kwa kujenga kiwanda kikubwa sana Katika mkoa wa Mtwara na kufanya Tanzania kua nchi yenye kiwanda kikubwa sana ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati,  pia  Bilionea uyo inasadikika kua mwaka 2016 amepoteza zaid ya Dolla Billion 4.4  kutokana Na kushuka kwa Saruji Nigeria, Bilionea uyo shabiki mkubwa wa Arsenal, ameahid kuinunua timu iyo baada ya miaka minne au mitatu na kusisitiza kua pesa kwake si tatizo kabsa katika kipind cha TV alichofanya Nchin Nigeria,, kwa muujibu wa orodha iliyotolewa na Bloomberg New York Nchin Marekani inaonyesha anautajili wa Dolla Billion 10.9 ambao unamuwezesha kabsa kumfanya chochote na kununua chochote Dunia hapa ameahid kuinunua timu iyo kwan yeye n shabiki mkubwa sana wa Arsenal,,,, Aliko Dangote Muislamu kutoka Nigeria alizaliwa 10/4/1957   pia kiwanda chake Tanzania ndio kinaongoza kwa kumiliki magari mengi na k

USHINDI WAANZA KUONEKANA GABON


AFCON imeanza kunogA uko GABON, Algeria na Tunisia zilitoka sale ya mabao. Mwili kwa. Mawili mechi ilkua ngumu  na kwel siku zote mwanzo mtamu mechi ilikua ngumu pande zote kwingineko Senegal waliichalaza Tunisia mabao Mawili kwa bila , ivyo mechi hizo zimekamilisha michezo ya kund B, ngoma bado tamu na ngumu pande zote michezo itaendelea kwa kundi C, kaa na infomer wako LUI nkupe stori njema

Jumapili, 15 Januari 2017

AFCON GABON NGOMA BADO NZITO


Kombe la mataifa AFRIKA mechi zilizokwisha pgwa, ila ngoma bado ngumu kwa kila timu kwani droo zimetawala na kila timu inaonekana kujiandaa vizuri

BAADA YA MUNGU Ni MZUNGU TEKNOLOJIA INAKUA KWA SPEED KILA SiKU CHECK HII



Ukuaji wa teknolojia umekua ukikua siku adi siku, na kurahisisha vitu vingi sana, teknolojia inakua kwa speed sana hasa kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi, mpango wa nchi zilizoendelea ni kwamba kufika mwaka 2050 watu wawe manaongoza tu na co kufanya chochote yaan kila mtu awe meneja na mashine zifanye kila kitu, teknolojia sasa imekuja na saa ambayo inaweza kutumika kama simu na kifaa chakuifadhia vitu pia kwan inaweka memory care na lain pia na uwezo wakuunganisha na simu aina yoyote windows, I phone Android na simu yoyote yenye uwezo wa bluetooth zimeshafika Tanzania ukiitaji nichek