Jumatano, 20 Septemba 2017
WASANII BONGO NA UPENDO WA MACHONI
Prodyuza wa THT, Emma The Boy, ambaye alipotea kwa takribani siku tano ila kwa sasa ameshapatikana, lakini cha ajabu wasanii wa Bongo fleva walikaa kimya, kama vile hawajui au haiwahusu, jambo hili linaonyesha wazi ndani ya tasnia yenu kuna ubaguzi.
Maswali ninayojiuliza hadi sasa ni kwanini alivyotekwa Roma mlihangaika usiku na mchana? Mkapaza sauti zenu kupitia mitandao yenu ya kijamii na mkashinda vituo vya polisi na mahospitalini? Mkaitisha mkutano wa kujadiliana juu ya nini cha kufanya?, kwa takribani siku mbili hakukuwa na stori nyingine zaidi ya huzuni tu.
Na kwa kiasi kikubwa zenu zilizaa matunda na hatimaye Roma, moni na bin laden wakapatikana, ndiyo maana kwa kulitambua hilo kupitia ngoma yake za Zimbabwe akawashukuru wale wote waliopaza sauti zao.
Lakini juhudi hizo mlishindwa kuzionyesha kwenye tukio la Emma The Boy, ambalo linafanana na lile la Roma, siyo mitandaoni, wala kikao cha kujadili mtampata wapi, ndiyo kwanza mpo bize na mambo yenu, kwani yeye na Roma wana tofauti gani?, ni kwamba taarifa hamkuzisikia au haikuwagusa ndiyo maana mliwasusia wasanii wa THT tu, wakiwemo Ditto, Amini na Barnaba ndiyo wahangaike peke yao?,
nlichogundua ni kama umoja wa usoni tu ila moyoni hamna kitu nakumbuka pia kifo cha NGWEA kila mtu aliuzunika na mlijitolea kweli ajabu ni kifo cha LANGA ambacho kilikua siku kadhaa tu baada ya kifo cha Ngwea lakin cha ajabu mapokeo hayakua kama ya Albert Mangwea , tasnia yetu ina shida flani ambayo hatuijui sema mungu atusaidie lipite mbali
Neno langu co sheria, lakin poleni kama nimewakela
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni