Alhamisi, 21 Septemba 2017
MADEE NA DOGO JANJA KUJA NA ALBUM YA PAMOJA ; MADO
Wasanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee na Dogo Janja wana mpango wa kutoa albamu ya pamoja.kabla ya mwaka huu kuisha .
Dogo Janja ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa album hiyo itakwenda kwa jina la Mado ikiwa ni muunganiko wa majina yao na wanatarajia kuitoa November mwaka huu.
“Album itakuja inaitwa MADO ni yangu na na Madee, unajua album ni stori, ni kama kitabu unatakiwa ukisikiliza uelewe, siyo tu nyimbo ndio maana ukifuatilia Machozi, Jasho na Damu imeelezea tu,” amesema Dogo Janja.
Mwaka huu tumeona baadhi ya wasanii wa bpngo flava wakijinadi kutoa album swala ninalo lisubiliwa kwa hamu na watu wengi, mimi kama mdau wa muziki nafurahi kuckia ivyo ,miaka ya hivi karibuni album zimeonakana kua ngumu sana kuuzika yote kutokana na teknolojia ya internent kurahisisha mfumo wa upatikanaji, miongoni mwa wasanii walio dhibitisha kutoa album mwaka huu ni pamoja na CHEGE CHIGUNDA, FID Q , ROMA NA STAMINA,NA BARNABA mashabiki tunasubili kwa hamu kubwa ujio wa hizi album
.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni