Maendeleo jijini mwanza yanakua kwa kasi sana katika nyanja nyingi hasa kiuchumi na kijamii , maendeleo yanakua kwa kasi sana kila kukicha kwani Mwanza ya kitambo co sawa na Mwanza ya sasa mbali na Ziwa Victoria kua n moja ya vivutio vizuri kuwahi kuwepo jijini humo pia miundombinu imezidi kuboreshwa kila siku iendayo kwa Mungu . Ukirudi miaka mitano nyuma utakubaliana na mm kua Mwanza ya sasa imebadilika sana kwa nyanja mbali mbali barabara karbia zote mjini kati zina lami hali inayozidi kuunyanyua uchumi kwa kasi sana..
Upanuzi wa barabara mbalimbali kati kati ya jiji umezidi kupendezesha na kurahisisha usafili hali inayopelekea kukua kwa uchumi jijini hapa , upanuzi wa barabara nne makongoro mpaka Airport unazidi kunogesha maadhali ya jiji letu au upanuzi wa barabara tatu kati ya Mlango mmoja mpaka Igoma unazidi kufanya jiji kuonekana zuri kila kukicha. Leo ndugu yenu wa damu kabsa nmeamua kuwaleetea maeneo matano (5) ambayo ni vyepesi sn kuishi hasa mtu wa kipato cha kawaida au kipato cha chini . Ifuatayo ni list ya maeneo matano mepesi kuishi jijini Mwanza, na ntaanza na no 5 mpaka 1..
5: BUHONGWA
Hii ni seemu ya wilaya Nyamagana , pia ni kituo kikuu cha daladala zitokazo mjini kwenda Buhongwa , seem hii imechangamka sana pia inafursa za kazi na kujiajili.pia , kuna soko kubwa la mazao ya chakula na wakazi wengi wa eneo hili ni watu wa kipato cha chini kuanzia (500) unapata chakula na unaishi vizur ivyo kija yoyote , unaweza kuchukua km fursa iv ili kuendeleza harakati zako town...
4:IGOMA
Uku ni Wilaya ya Nyamagana kama kilometa 11 kutoka mjini kati , kuna machinjio kubwa Mwanza nzima ipo maeneo haya pia wepesi wa upatikanaji vitu ni mkubwa sn kwani kuna adi nguo za buku buku sharti nzuri tu unapata pia kuna uwepesi wa vyakula na fursa za ajira zipo nyingi sn kwani kuna viwanda vingi sn maeneo jiran km kijereshi na mnadani , mbali na fursa zilizopo pia ndo eneo ambalo linaongoza kua na wasukuma wengi sn jijini Mwanza , pia kuna mnada wa Ng"ombe na Mbuzi hali inayofanya pazidi kua na fursa nying za ajira , Vyumba adi elfu kumi unapata so km umechoka kukaa kwa Mama ni moja ya maeneo mazur sana kwa kuanzia maisha kwani kuna wepesi wakuishi ...
3:PASIANSI NA MABATINI
Pasiansi ipo wilaya ya Ilemela ni eneo la makutano ya Kiloleli , Airport na Mjini kati kuna mihangaiko mingi sn usiku na mchana pia ni sehemu nyepesi kuishi kwani kuna miundombinu inayowakutanisha watu pamoja pia kuna Hotel kubwa km Lenana ambayo ni nyota tano , Mabatini ni km Kilometa 2 iv kutoka mjini ni sehemu nzuri kuishi kwa kipato chakuanzia maisha pia ni sehemu nzuri kuwekeza kama una mtonyo ivi,, maisha yanawepesi sn kwani ata elfu kumi unapata chumba , so mdau ukimchoka mama.njoo uku kwetu, Ndo maana sisi tunapaita Califonia kwani pako km blooklyne iv au Los Angels
2:KIRUMBA
Eneo lipo maeneo ya Ilemela karbu kabsa na Ziwa victoria Km 2 kutoka mjini kati mbali ya kua ndo eneo ilipo soko kubwa la samaki jijini Mwanza ila pia ndo eneo lenye Garage nyingi na Hotel nying sn Kirumba huchangamka 24/7 , yaani masaa 24 ndani ya siku 7 za wiki kwa Mwanza hili ndo eneo ambalo la kwanza kwanza kua na Hotel na Disco la kisasa kabsa maeneo kama Villa Park Resort La kailo ni moja ya sehemu nzuri kabsa za starehe kuanzishwa jijini hapa km umefika mwanza na una weweseka pakuwekeza njoo uku panakufaaaa sn....
Namba 1 ni NYAKATO NA NYEGEZI Nyakato ni sehemu iliyochangamka sn jijini Mwanza mishemishe za hela ni kubwa na nyingi sana kwani wingi wa watu hufanya paonekane kama mbele yaani kuna stand kubwa ya magar ya mkoani pia kuna miundombinu mizuri kwani kuna barabara ya makutano kati ya Musoma , Mjini kati na Kilimahewa , ni moja ya sehemu nzur Mwanza, Nyegezi ni moja ya sehemu zilizochagamka kuanzia watu wenyewe na fursa zilizopo kuna stand ya magari ya mkoani hali inayoiyfanya kua na fursa nyingi sn za kujiajili na kuishi hasa km ni kijana unaeanza maisha, Kama mgeni lazma uenjoy sn au hata mwenyeji .
Kama ni mgeni jijini au mwenyeji najua ukifika maeneo hayo lazma ukubakiane na mimi , yapo maeneo mengi sana ila haya ni baadhi tu ya maeneo ambayo mimi nayakubali cku zote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni