Alhamisi, 21 Septemba 2017
NICKY MINAJ KAINGIZA RASMI BIDHAA YAKE YA LIPSTIC SOKONI
Rapper wa kike kutoka Young Money Nicki Minaj amekuja lipstik yake baada ya kutangaza kuachia rasmi bidhaa zake hizo sokoni mwezi huu.
Nicki ambaye alitangaza kuachia bidhaa hizo mwezi uliopita kupitia kampuni ya M.A.C amefanya hivyo kwa kuachia aina mbili za lipstick ambazo ni NickisNude na ThePinkprint, zitakazouzwa kuanzia dola 18 sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi elfu arobaini ivi za kibongo 40,000\=
“Ok I’m about to announce my winners on twitter. This might be the illest gift set I’ve ever seen. My fans deserve it. They’re gonna be so happy. But mad jealous too if they don’t win. Awww @maccosmetics you’re getting like 20 lipsticks and 2 glosses. Yikes. Plus my signature colors #ThePinkprint & #NickisNude We’ve officially launched in the US!!!!!!,” ameandika mrembo huyu kupitia mtandao wa Instagram.
uwekezaji uleta matokeo mazuri ra badae ata TANZANIA tumemuona Nasibu Abdul Diamond akiwa msanii wakwanza Tanzania kufanya uwekezaji mkubwa katika perfume zake aina ya Chibu perfume na Karanga , ambapo bidhaa zote zinaonyesha kufanya vizuri sokoni , msanii mwingne kutoka bongo ambaye ame anauwekezaji kama huo ni Joh makini ambae bado haijawa officil ila ana tarajia kuachia condom zake MAKINI condom
HIP HOP YANGU INAPEDWA KULIKO WANAOJIITA WANA HIP HOP; NAY
Msanii wa muziki wa Bongo, Nay wa Mitego wamejitapa na kujivunia style yake ya muziki anayofanya licha ya baadhi ya wasanii wenzake kumuondoa katika kundi la wasanii wa hip hop.
Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuondolewa katika kundi la muziki wa HIP HOP hakumuumizi kwani anaangalia biashara na wasanii wanatakiwa washindane katika eneo hilo.
“Muziki wa HIP HOP unahitaji vitu ambavyo vinaishi, tuzungumzie maisha ya watu ya kila siku. Utaona wanasema Nay siyo mwanahip hop, wananitoaga kwenye kundi la hip hop lakini why ndio na mashabiki wengi kuliko wao, why nimekuwa napendwa kuliko wao, why angalau na vijihatua kuliko wao?” amesema Nay.
“Ni kwa sababu nafanya kitu cha Watanzania nafanya kitu ambacho kipo kwa wakati huo na ndivyo tunatakiwa kufanya ili isionekane kila siku waimbaji ndio wana mkwanja, tushindane. Marekani wasanii wenye hela nyingi ni wanahip hop kwanini na sisi tusiweze hivyo,” ameongeza.
Kwa mwaka huu Nay wa Mitego ametoa ngoma kama Wapo na Moto ambazo zipo katika style ya rap, huku ngoma kama Makuzi na Acheze zikiwa katika style ya kuimba.
NAY ni moja ya wasanii ambao walianza na muziki wa HIP HOP kutokana na ugumu kwamba mziki huo hauna soko hapa bongo na kuanza kuimba imekua changamoto kubwa kwa wasanii wengi sana nchini hapa asilimia 90 ya wasanii wa HIP HOP wamebadilisha muziki wao kwa madai muziki huo haulipi , miongoni mwa wasanii walio wahi kuchana ila sasa ni waimbaji ni MADEE, DIAMOND, DULLY SYKES, RAYVANNY, NA wengine wengi
ila wachache kama FID Q, CHINDO, wanaonekana kua baadhi wasanii walio baki kwenye misingi ya HIP HOP BONGO
MADEE NA DOGO JANJA KUJA NA ALBUM YA PAMOJA ; MADO
Wasanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee na Dogo Janja wana mpango wa kutoa albamu ya pamoja.kabla ya mwaka huu kuisha .
Dogo Janja ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa album hiyo itakwenda kwa jina la Mado ikiwa ni muunganiko wa majina yao na wanatarajia kuitoa November mwaka huu.
“Album itakuja inaitwa MADO ni yangu na na Madee, unajua album ni stori, ni kama kitabu unatakiwa ukisikiliza uelewe, siyo tu nyimbo ndio maana ukifuatilia Machozi, Jasho na Damu imeelezea tu,” amesema Dogo Janja.
Mwaka huu tumeona baadhi ya wasanii wa bpngo flava wakijinadi kutoa album swala ninalo lisubiliwa kwa hamu na watu wengi, mimi kama mdau wa muziki nafurahi kuckia ivyo ,miaka ya hivi karibuni album zimeonakana kua ngumu sana kuuzika yote kutokana na teknolojia ya internent kurahisisha mfumo wa upatikanaji, miongoni mwa wasanii walio dhibitisha kutoa album mwaka huu ni pamoja na CHEGE CHIGUNDA, FID Q , ROMA NA STAMINA,NA BARNABA mashabiki tunasubili kwa hamu kubwa ujio wa hizi album
.
Jumatano, 20 Septemba 2017
WASANII BONGO NA UPENDO WA MACHONI
Prodyuza wa THT, Emma The Boy, ambaye alipotea kwa takribani siku tano ila kwa sasa ameshapatikana, lakini cha ajabu wasanii wa Bongo fleva walikaa kimya, kama vile hawajui au haiwahusu, jambo hili linaonyesha wazi ndani ya tasnia yenu kuna ubaguzi.
Maswali ninayojiuliza hadi sasa ni kwanini alivyotekwa Roma mlihangaika usiku na mchana? Mkapaza sauti zenu kupitia mitandao yenu ya kijamii na mkashinda vituo vya polisi na mahospitalini? Mkaitisha mkutano wa kujadiliana juu ya nini cha kufanya?, kwa takribani siku mbili hakukuwa na stori nyingine zaidi ya huzuni tu.
Na kwa kiasi kikubwa zenu zilizaa matunda na hatimaye Roma, moni na bin laden wakapatikana, ndiyo maana kwa kulitambua hilo kupitia ngoma yake za Zimbabwe akawashukuru wale wote waliopaza sauti zao.
Lakini juhudi hizo mlishindwa kuzionyesha kwenye tukio la Emma The Boy, ambalo linafanana na lile la Roma, siyo mitandaoni, wala kikao cha kujadili mtampata wapi, ndiyo kwanza mpo bize na mambo yenu, kwani yeye na Roma wana tofauti gani?, ni kwamba taarifa hamkuzisikia au haikuwagusa ndiyo maana mliwasusia wasanii wa THT tu, wakiwemo Ditto, Amini na Barnaba ndiyo wahangaike peke yao?,
nlichogundua ni kama umoja wa usoni tu ila moyoni hamna kitu nakumbuka pia kifo cha NGWEA kila mtu aliuzunika na mlijitolea kweli ajabu ni kifo cha LANGA ambacho kilikua siku kadhaa tu baada ya kifo cha Ngwea lakin cha ajabu mapokeo hayakua kama ya Albert Mangwea , tasnia yetu ina shida flani ambayo hatuijui sema mungu atusaidie lipite mbali
Neno langu co sheria, lakin poleni kama nimewakela
LISU INABIDI APELEKWE MAREKANI; NYALANDU
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweka kambi nchini Kenya kuangalia uwezokano wa kupata ruhusa kutoka kwa madaktari ya kumsafirisha Mh Tundu Lissu kwenda Marekani kwaajili ya matibabu zaidi baada kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Nyalandu amedai ni siku ya tatu bado hajapata ripoti inayoonyesha maendeleo ya mgonjwa huyo ili waangalie kama wanaweza kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi.
Taarifa ya Mh Nyalandu
Tumekuwa Nairobi Hospital tukisubiri madaktali watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissukupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospitalwangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)








