Alhamisi, 26 Oktoba 2017

JARIDA MAARUFU NIRIA LAMPA SHAVU PETER

Jarida la Vibe.ng kutoka nchini Nigeria limempa shavu msanii wa muziki Peter aliyekuwa moja ya memba wa kundi la P-Square, linalounda na yeye pamoja na pacha wake Paul. Kupitia jarida hilo linalotarajiwa kutoka hivi karibuni, Peter ama Mr.P amefunguka mengi ikiwemo kutochanganya biashara na masuala ya familia, vile vile ameelezea juu ya kuvunjika kwa kundi hilo ambalo limefanya kazi kwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10. “One thing I will never do when I come back to this life again is mix family with business,” Peter Okoye, now known as Mr P, says as he discusses the break up of P-Square,’’ ameleza Peter kupitia jarida hilo la Vibe. Kwa sasa Peter anafanya kazi zake binafsi na amesha achia video yake ya kwanza iitwayo ‘Cool It Down’wiki moja iliyopita. Baadhi ya picha zinazopatikana katika jarida hilo.

Alhamisi, 21 Septemba 2017

NICKY MINAJ KAINGIZA RASMI BIDHAA YAKE YA LIPSTIC SOKONI

Rapper wa kike kutoka Young Money Nicki Minaj amekuja lipstik yake baada ya kutangaza kuachia rasmi bidhaa zake hizo sokoni mwezi huu. Nicki ambaye alitangaza kuachia bidhaa hizo mwezi uliopita kupitia kampuni ya M.A.C amefanya hivyo kwa kuachia aina mbili za lipstick ambazo ni NickisNude na ThePinkprint, zitakazouzwa kuanzia dola 18 sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi elfu arobaini ivi za kibongo 40,000\= “Ok I’m about to announce my winners on twitter. This might be the illest gift set I’ve ever seen. My fans deserve it. They’re gonna be so happy. But mad jealous too if they don’t win. Awww @maccosmetics you’re getting like 20 lipsticks and 2 glosses. Yikes. Plus my signature colors #ThePinkprint & #NickisNude We’ve officially launched in the US!!!!!!,” ameandika mrembo huyu kupitia mtandao wa Instagram.
uwekezaji uleta matokeo mazuri ra badae ata TANZANIA tumemuona Nasibu Abdul Diamond akiwa msanii wakwanza Tanzania kufanya uwekezaji mkubwa katika perfume zake aina ya Chibu perfume na Karanga , ambapo bidhaa zote zinaonyesha kufanya vizuri sokoni , msanii mwingne kutoka bongo ambaye ame anauwekezaji kama huo ni Joh makini ambae bado haijawa officil ila ana tarajia kuachia condom zake MAKINI condom

HIP HOP YANGU INAPEDWA KULIKO WANAOJIITA WANA HIP HOP; NAY

Msanii wa muziki wa Bongo, Nay wa Mitego wamejitapa na kujivunia style yake ya muziki anayofanya licha ya baadhi ya wasanii wenzake kumuondoa katika kundi la wasanii wa hip hop. Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuondolewa katika kundi la muziki wa HIP HOP hakumuumizi kwani anaangalia biashara na wasanii wanatakiwa washindane katika eneo hilo. “Muziki wa HIP HOP unahitaji vitu ambavyo vinaishi, tuzungumzie maisha ya watu ya kila siku. Utaona wanasema Nay siyo mwanahip hop, wananitoaga kwenye kundi la hip hop lakini why ndio na mashabiki wengi kuliko wao, why nimekuwa napendwa kuliko wao, why angalau na vijihatua kuliko wao?” amesema Nay. “Ni kwa sababu nafanya kitu cha Watanzania nafanya kitu ambacho kipo kwa wakati huo na ndivyo tunatakiwa kufanya ili isionekane kila siku waimbaji ndio wana mkwanja, tushindane. Marekani wasanii wenye hela nyingi ni wanahip hop kwanini na sisi tusiweze hivyo,” ameongeza. Kwa mwaka huu Nay wa Mitego ametoa ngoma kama Wapo na Moto ambazo zipo katika style ya rap, huku ngoma kama Makuzi na Acheze zikiwa katika style ya kuimba. NAY ni moja ya wasanii ambao walianza na muziki wa HIP HOP kutokana na ugumu kwamba mziki huo hauna soko hapa bongo na kuanza kuimba imekua changamoto kubwa kwa wasanii wengi sana nchini hapa asilimia 90 ya wasanii wa HIP HOP wamebadilisha muziki wao kwa madai muziki huo haulipi , miongoni mwa wasanii walio wahi kuchana ila sasa ni waimbaji ni MADEE, DIAMOND, DULLY SYKES, RAYVANNY, NA wengine wengi ila wachache kama FID Q, CHINDO, wanaonekana kua baadhi wasanii walio baki kwenye misingi ya HIP HOP BONGO

MADEE NA DOGO JANJA KUJA NA ALBUM YA PAMOJA ; MADO

Wasanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee na Dogo Janja wana mpango wa kutoa albamu ya pamoja.kabla ya mwaka huu kuisha . Dogo Janja ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa album hiyo itakwenda kwa jina la Mado ikiwa ni muunganiko wa majina yao na wanatarajia kuitoa November mwaka huu. “Album itakuja inaitwa MADO
ni yangu na na Madee, unajua album ni stori, ni kama kitabu unatakiwa ukisikiliza uelewe, siyo tu nyimbo ndio maana ukifuatilia Machozi, Jasho na Damu imeelezea tu,” amesema Dogo Janja. Mwaka huu tumeona baadhi ya wasanii wa bpngo flava wakijinadi kutoa album swala ninalo lisubiliwa kwa hamu na watu wengi, mimi kama mdau wa muziki nafurahi kuckia ivyo ,miaka ya hivi karibuni album zimeonakana kua ngumu sana kuuzika yote kutokana na teknolojia ya internent kurahisisha mfumo wa upatikanaji, miongoni mwa wasanii walio dhibitisha kutoa album mwaka huu ni pamoja na CHEGE CHIGUNDA, FID Q , ROMA NA STAMINA,NA BARNABA mashabiki tunasubili kwa hamu kubwa ujio wa hizi album .

Jumatano, 20 Septemba 2017

WASANII BONGO NA UPENDO WA MACHONI

Prodyuza wa THT, Emma The Boy, ambaye alipotea kwa takribani siku tano ila kwa sasa ameshapatikana, lakini cha ajabu wasanii wa Bongo fleva walikaa kimya, kama vile hawajui au haiwahusu, jambo hili linaonyesha wazi ndani ya tasnia yenu kuna ubaguzi. Maswali ninayojiuliza hadi sasa ni kwanini alivyotekwa Roma mlihangaika usiku na mchana? Mkapaza sauti zenu kupitia mitandao yenu ya kijamii na mkashinda vituo vya polisi na mahospitalini? Mkaitisha mkutano wa kujadiliana juu ya nini cha kufanya?, kwa takribani siku mbili hakukuwa na stori nyingine zaidi ya huzuni tu. Na kwa kiasi kikubwa zenu zilizaa matunda na hatimaye Roma, moni na bin laden wakapatikana, ndiyo maana kwa kulitambua hilo kupitia ngoma yake za Zimbabwe akawashukuru wale wote waliopaza sauti zao. Lakini juhudi hizo mlishindwa kuzionyesha kwenye tukio la Emma The Boy, ambalo linafanana na lile la Roma, siyo mitandaoni, wala kikao cha kujadili mtampata wapi, ndiyo kwanza mpo bize na mambo yenu, kwani yeye na Roma wana tofauti gani?, ni kwamba taarifa hamkuzisikia au haikuwagusa ndiyo maana mliwasusia wasanii wa THT tu, wakiwemo Ditto, Amini na Barnaba ndiyo wahangaike peke yao?, nlichogundua ni kama umoja wa usoni tu ila moyoni hamna kitu nakumbuka pia kifo cha NGWEA kila mtu aliuzunika na mlijitolea kweli ajabu ni kifo cha LANGA ambacho kilikua siku kadhaa tu baada ya kifo cha Ngwea lakin cha ajabu mapokeo hayakua kama ya Albert Mangwea , tasnia yetu ina shida flani ambayo hatuijui sema mungu atusaidie lipite mbali Neno langu co sheria, lakin poleni kama nimewakela

LISU INABIDI APELEKWE MAREKANI; NYALANDU

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweka kambi nchini Kenya kuangalia uwezokano wa kupata ruhusa kutoka kwa madaktari ya kumsafirisha Mh Tundu Lissu kwenda Marekani kwaajili ya matibabu zaidi baada kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Nyalandu amedai ni siku ya tatu bado hajapata ripoti inayoonyesha maendeleo ya mgonjwa huyo ili waangalie kama wanaweza kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi. Taarifa ya Mh Nyalandu Tumekuwa Nairobi Hospital tukisubiri madaktali watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissukupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospitalwangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo

Jumatatu, 17 Julai 2017

MCHORO WENYE DHAMANI KUBWA KUWAHI KUTOKEA DUNIANI

Kama wewe ni mbukuzi kama mimi hapa nadhani ushawahi kusikia au kuona (kwenye runinga) mchoro maarufu wa MONALISA mchoro wenye dhamani kubwa sana Dunia nzima ambao watu husafiri kutoka nchi mbali mbali kwenda kuuona nchini ITALY katika makumbusho ya LOUVRE ambapo unadhamani ya Dolla millioni 785 iv , ni pesa nyingi sana , na watu mbali mbali husafili kwenda Ufaransa kuuona , una ulinzi wa Hali ya juu kwani watu kadhaa walijalibu kuuiba miaka ya nyuma . Mchoro huu ndo mchoro maarufu sana kuwahi kutokea Duniani ..

HISTORIA FUPI
Mchoro wa MONALISA ulichorwa na Leonardo Da Vinci raia wa Italy aliezaliwa 15.4.1452 hukoo nchini Italy , Leonardo ni moja ya watu makini kuwahi kutokea duniani kwani ana nadhalia zake ambazo mpaka kesho zinatumiwa sana duniani , hakuwa tu mchoraji pia alikua Mwanasayansi, Mwanahisabati, Mwanamuziki, na fani nyingine mbali mbali ndo maana wahenga kama mimi tunamuona ni moja ya ma geneus kuwahi kutokea , ikumbukwe Leonardo ndo mtunzi au msimamizi wa Nadhalia ya sayansi ya kitu kupaa angani bila kushika mahali na ndo maana hufananishwa sana na watu kama Isaac Newton, Albert Einstein, Galileo Socrates n.k Uchoraji wa picha ya MONALISA ulianza mwaka 1503 mpaka 1506 , alipoukamilisha kwa kiasi kikubwa sana , mnamo mwaka huo huo alihamia Ufaransa na kuendelea na makazi yake kule , mchoro wa MONALISA haukua mchoro wa siku wiki au mwez ulichukua mda sana , kwakua Mchoraji Leonardo alikua akijihusisha na mambo mengi ilimchukua mda sana na inaaminika ndo sababu ya picha kua nzuri adi kesho kutwa kwani ilichukua mda sanaa. Mnamo tarehe 2.5.1519 umauti ulimfika Leonardo Da Vinci mchoraji wa mchoro wa MONALISA ulikua wakawaida sana ila vitu vilivyofanya mchoro huu kua special ni kutokana na mtu mwenyewe aliemchora kua special sana katika maisha ya kawaida ..

Baada ya miaka 300 baada ya kifo cha Leonardo picha ilianzakujipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na ustadi uliokua umetumika kuichora picha ile ule upekee wa picha na uhalisia uliifanya picha ile kuonekana special sana karne ya 19 watoto wa wafalme mbali mbali duniani waliitumia picha ile km mifano ya wanawake ambao wanatamani kuwaowa .

Salai mwanafunzi wa Leonardo alitumia picha ile kujipatia kipato kwa kuionyesha sehemu mbali mbali mnamo karne ya 19 watu mbali mbali walisafiri kwenda kuiona picha iyo ilizidi kujipatia umaarufu mwaka 1963  Rais wa Marekani kwa kipindi kile John F. Kennedy aliiomba picha iyo iende marekani na ililindwa sn na kukatiwa bima ya dolla million 600 , iliwasili nchini Marekani Washingtoni DC na watu na misululu miref ilisimamwa pale watu kuishika tu na kila mtu aliishika kwa sekunde 15 tu . Mwaka 1964 nchi kama Japani na USSR ,nazo zilizidi kuipa umaarufu sana picha ile kwani ilitakiwa kuenda pia kwa nchi hizo.

UPEKEE WA PICHA

1;Ndo ilikua picha ya kwanza ya rangi kuchorwa kwakipindi kile miaka ilipo chorwa.

2; Ulikua ni mchoro mzuri wa mtu wakusadikika ambae kila mwanaume alitamani kua na Mwanamke kama yeye na wakati hakuwepo wala hakuwahi kutokea

3; Picha ya MONALISA ilimuonyesha mwanamke mzuri ila hakuwa na Nyusi wala kidani chochote ila alikua mzuri sana .

4;Mchoraji mwenyewe Leonardo Da Vinci alikua ni moja ya ma genious wachache kuwahi kutokea Duniani .

5; Ndo picha yenye dhamani kubwa Dunia nzima adi hii leo

Iliwahi kuibiwa mwaka 1856 ila waliipata 1857 na watu wengi waliona kua picha iyo inadhamani kubwa adi hii leo inaulinzi wa bullet proof ndani ya makumbusho ya Louvre Paris nchini Ufaransa  .

By FOBES