Kama wewe ni mbukuzi kama mimi hapa nadhani ushawahi kusikia au kuona (kwenye runinga) mchoro maarufu wa MONALISA mchoro wenye dhamani kubwa sana Dunia nzima ambao watu husafiri kutoka nchi mbali mbali kwenda kuuona nchini ITALY katika makumbusho ya LOUVRE ambapo unadhamani ya Dolla millioni 785 iv , ni pesa nyingi sana , na watu mbali mbali husafili kwenda Ufaransa kuuona , una ulinzi wa Hali ya juu kwani watu kadhaa walijalibu kuuiba miaka ya nyuma . Mchoro huu ndo mchoro maarufu sana kuwahi kutokea Duniani ..
HISTORIA FUPI
Mchoro wa MONALISA ulichorwa na Leonardo Da Vinci raia wa Italy aliezaliwa 15.4.1452 hukoo nchini Italy , Leonardo ni moja ya watu makini kuwahi kutokea duniani kwani ana nadhalia zake ambazo mpaka kesho zinatumiwa sana duniani , hakuwa tu mchoraji pia alikua Mwanasayansi, Mwanahisabati, Mwanamuziki, na fani nyingine mbali mbali ndo maana wahenga kama mimi tunamuona ni moja ya ma geneus kuwahi kutokea , ikumbukwe Leonardo ndo mtunzi au msimamizi wa Nadhalia ya sayansi ya kitu kupaa angani bila kushika mahali na ndo maana hufananishwa sana na watu kama Isaac Newton, Albert Einstein, Galileo Socrates n.k Uchoraji wa picha ya MONALISA ulianza mwaka 1503 mpaka 1506 , alipoukamilisha kwa kiasi kikubwa sana , mnamo mwaka huo huo alihamia Ufaransa na kuendelea na makazi yake kule , mchoro wa MONALISA haukua mchoro wa siku wiki au mwez ulichukua mda sana , kwakua Mchoraji Leonardo alikua akijihusisha na mambo mengi ilimchukua mda sana na inaaminika ndo sababu ya picha kua nzuri adi kesho kutwa kwani ilichukua mda sanaa. Mnamo tarehe 2.5.1519 umauti ulimfika Leonardo Da Vinci mchoraji wa mchoro wa MONALISA ulikua wakawaida sana ila vitu vilivyofanya mchoro huu kua special ni kutokana na mtu mwenyewe aliemchora kua special sana katika maisha ya kawaida ..
Baada ya miaka 300 baada ya kifo cha Leonardo picha ilianzakujipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na ustadi uliokua umetumika kuichora picha ile ule upekee wa picha na uhalisia uliifanya picha ile kuonekana special sana karne ya 19 watoto wa wafalme mbali mbali duniani waliitumia picha ile km mifano ya wanawake ambao wanatamani kuwaowa .
Salai mwanafunzi wa Leonardo alitumia picha ile kujipatia kipato kwa kuionyesha sehemu mbali mbali mnamo karne ya 19 watu mbali mbali walisafiri kwenda kuiona picha iyo ilizidi kujipatia umaarufu mwaka 1963 Rais wa Marekani kwa kipindi kile John F. Kennedy aliiomba picha iyo iende marekani na ililindwa sn na kukatiwa bima ya dolla million 600 , iliwasili nchini Marekani Washingtoni DC na watu na misululu miref ilisimamwa pale watu kuishika tu na kila mtu aliishika kwa sekunde 15 tu . Mwaka 1964 nchi kama Japani na USSR ,nazo zilizidi kuipa umaarufu sana picha ile kwani ilitakiwa kuenda pia kwa nchi hizo.
UPEKEE WA PICHA
1;Ndo ilikua picha ya kwanza ya rangi kuchorwa kwakipindi kile miaka ilipo chorwa.
2; Ulikua ni mchoro mzuri wa mtu wakusadikika ambae kila mwanaume alitamani kua na Mwanamke kama yeye na wakati hakuwepo wala hakuwahi kutokea
3; Picha ya MONALISA ilimuonyesha mwanamke mzuri ila hakuwa na Nyusi wala kidani chochote ila alikua mzuri sana .
4;Mchoraji mwenyewe Leonardo Da Vinci alikua ni moja ya ma genious wachache kuwahi kutokea Duniani .
5; Ndo picha yenye dhamani kubwa Dunia nzima adi hii leo
Iliwahi kuibiwa mwaka 1856 ila waliipata 1857 na watu wengi waliona kua picha iyo inadhamani kubwa adi hii leo inaulinzi wa bullet proof ndani ya makumbusho ya Louvre Paris nchini Ufaransa .
By FOBES